LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 2, 2019

JPM AMTEUA PROF. KAHIMBA KUWA MKURUGENZI MKUU TEMDO.


Ikulu, Dar es Salaam.

RAIS Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Fredrick Cassian Kahimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kahimba umeanza tarehe 31 Agosti, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kahimba alikuwa Profesa Mshiriki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.

Prof. Kahimba amechukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages