Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 324 na kuwajeruhi wengine 18,000 katika maandamano ya amani ya 'Haki ya Kurejea' ambayo hufanyika kila Ijumaa katika Ukanda wa Ghaza.
Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Haki za Binadamu cha Mizan Wapalestina hao wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika maandamano ambayo yalianza mwezi Machi mwaka 2018.
Ripoti hiyo imesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umekataa kukabidhi miili ya Wapalestina 16 waliouawa shahidi ambapo miongoni mwao kuna watoto watatu. Aidha kwa mujibu wa takwimu hizo za Wapalestina 324 waliouawa shahidi, 46 ni watoto, wanawake na vilema. Aidha miognoni mwa waliouawa shahidi ni wafanyakazi wanne wa sekta ya afya na waandishi habari wawili.
Hali kadhalika miongoni mwa Wapalestina 18,000 waliojeruhiwa, 4,438 ni watoto na 813 ni wanawake.
Maandamano makubwa ya "Haki ya Kurejea" yalianza tarehe 30 Machi mwaka uliopita wa 2018 kwa madhumuni ya kuhitimisha mzingiro wa miaka 13 liliowekewa eneo la Ukanda wa Gaza na kupinga kitendo cha Marekani cha kuuhamishia ubalozi wake katika mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem).
Maandamano makubwa ya Haki ya Kurejea hufanyika kila siku ya Ijumaa katika mpaka wa mashariki wa Ukanda wa Gaza na Israel (ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇