Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAMLAKA
ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendelea na ukaguzi
wa miundo mbinu ya maji inayohujumiwa na Wananchi wasio waaminifu.
Wananchi hao wamekuwa wanasababisha Mamlaka kupata hasara kubwa kwa kujiunganishia maji kwa njia ya wizi.
Zoezi la kuwabaini wahujumu wa miundo
mbinu ya maji linaendelea kwa mikoa ya kihuduma DAWASA ambapo Mkoa wa
Ubungo umeweza kubaini wizi wa maji kwa mteja asiye mwaminifu.
Akizungumzia zoezi hilo, Mwenyekiti wa
kampeni maalum ya kupambana na wahujumu wa huduma na miundombinu Ubungo
Frank Sulley amesema zoezi hilo limekua endelevu kwa Mkoa wa kihuduma
Ubungo na wameweza kuwabaini wananchi wasio waaminifu wanaosababisha
hasara kwa Mamlaka.
Amesema, wameweza kupata taarifa za
kiintelijensia usiku wa kuamkia tarehe 27 Septemba 2019, na kufanikiwa
kugundua wizi wa Maji eneo la Mbezi Inn alfajiri ya kuamkia tarehe 28
Septemba.
"Tuliweza kugundua hujuma iliyokua
ikifanyika na Mteja asiye mwaminifu kwa kujaza maji kwenye kisima
nyakati za usiku na na kuuza kwa Magari yanayofanya biashara ya kuuza
maji,"amesema Sulley.
Amesema, ni kosa kisheria kwa mwananchi
kujiunganishia maji na kuuza maji kwani hupunguzia Mamlaka Mapato na
Serikali kwa ujumla.
Sulley ameeleza, mwananchi atakapokamatwa
itapelekea kulipa faini isiyopungua milion 5 hadi milion 50 na ata
kufikishwa Mahakamani.
Ofisi ya kihuduma Mkoa wa Ubungo inapenda
kuwatahadharisha wananchi kuacha mara moja hujuma kwani hii ni hatari
kwa ustawi wa Dawasa na Serikali kwa ujumla.
Mwenyekiti wa kampeni maalum ya kupambana na wahujumu wa huduma na
miundombinu Mkoa wa Kihuduma Ubungo DAWASA, Frank Sulley akiwa na
wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa
miundo mbinu na kubaini mwananchi akihujumu kwa kujaza maji kwenhe
kisima na kuuza kwenye magari.
Mwenyekiti wa kampeni maalum ya kupambana
na wahujumu wa huduma na miundombinu Mkoa wa Kihuduma Ubungo DAWASA,
Frank Sulley akifungua kisima kinachodaiwa kujazwa maji na mwananchi na
kisha kuyauza kwenye magari. Wakati wa ukaguzi wa miundo mbinu ya DAWASA
ikiwa ni katika kupambana na wananchi wanaolihujumu Mamlaka.
Kisima kinachotumika na Mwananchi kujaza maji na kuyauza kwenye magari.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇