Wafanya
kazi wa Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania wamemuanga
Mkurungenzi wao anayeondoka kwa njia ya kipekee baada ya kuhudumu kwenye
kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka sita.
Akiongea
kwenye hafla hiyo, Mkurungenzi huyo anayeondoka Bw. Sunil Colaso
alisema kuwa Tanzania imekuwa ni kama nyumbani na hatua hii ya kuwaanga
ni ngumu kwani kwa kipindi cha miaka sita Tanzania imekuwa ni nyumbani.
“Nachukua
fursa hii kuwashukuru wafanya kazi wote wa Airtel kwa muda wote
tuliofanya kazi pamoja. Tumeshirikiana kufanya kazi kwa bidii na umoja
wenu ulifanya kazi yangu kuwa rahisi na kufanikisha malengo yetu. Ni
Imani yangu kuwa kuwa leo wakati naondoka ninaacha nyuma timu imara
ambayo itaendelea kuwahudumia Watanzania kwa huduma bora za mawasiliano
kila siku.
Alitoa
wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya
George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata
mafanikio makubwa zaidi ya haya.
Colaso pia akitoa shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania, Wizara na Taasisi zake zote kwa kuiunga mkono Airtel
Tanzania kwa kipindi chote cha uongozi wake. “nashukuru kwa dhati
serikali kwa kutuunga mkono Airtel Tanzania, ndio maana tumefanikiwa
kutoa huduma bora kimataifa na hapa nchni sana sana kwenye huduma za
Airtel Money, Airtel yatosha bando inayowafaidisha wateja kwa huduma za
kupiga simu pamoja na intaneti. Nawapongeza
pia wafanyakazi wote wa Airtel kwa kuwa na mafanikio ya kipekee ya
kuweza kusambaza huduma za Airtel Money mpaka vijijini ambapo hadi sasa
mmefungua zaidi ya maduka ya Airtel Money Branches 900. Alisema Colaso
Mkurungenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alimpongeza
Colaso huku akisema mbali ya bosi huyo kuwa ni mtu mwenye maono ya
kuendeleza sekta ya mawasiliano hapa nchini, lakini pia alijipambanua
katika kuifanya sekta ya mawasiliano kuleta tija katika maswala ya
uchumi hapa nchini.
“Tunamuaga
leo Mkurugenzi Sunil Colaso, alikuwa ni mtu wa kupenda kazi yake,
kujitolea kusaidiana na wafanyakazi kila alipohitajika, alipenda
kufanya kazi kwa Umoja, haya ni kati ya mambo ambayo tutamkumbuka
nayo. Alikuwa ni mtu mwenye sifa zote za kiongozi na mwenye kujenga timu
ya pamoja, alimpa kila mfanyakazi wa Airtel Tanzania nafasi ya
kuonyesha uwezo wake.’ Singano alieleza.
Mkurugenzi
wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akipokea keki kama ishara ya kuagana na
wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga ilifanyika
jijini Dar es salaam baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa
zaidi ya miaka 6.
Mkurugenzi
wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akikata keki kama ishara ya kuagana na
wafanyakazi wenzake wa Airtel katika hafla maalum kumuaga ilifanyika
jijini Dar es salaam baada ya kuiongoza Airtel Tanzania kwa muda wa
zaidi ya miaka 6.
Bw. Sunil Colaso ametoa
wito kwa wafanya kazi na wadau wengine kumuunga mkono Mkurugenzi mpya
George Mathen anayetarajiwa hapa nchini kuanzia mwezi ujao ili kupata
mafanikio makubwa zaidi ya haya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇