NA SALVATORY NTANDU
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamesherehekea sikukuu ya Eid Alhaj kwa kuwaombea watu wote walipoteza maisha na majeruhi katika ajali ya moto iliyohusisha lori la mafuta iliyotokea agosti 10 mwaka huu mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 75 huku 39 waliobaki wakiendelea kupatiwa matibabu.
Swala hiyo imeongozwa na mwakilishi wa jumuiya ya kisilamu ya Istiqama international wilayani humo Shekhe Ahmad Haroun Alnoob na kusema kuwa taifa bado linaendelea kuomboleza vifo vya watanzania wenzetu ambao wamefariki dunia kutokana ajali hivyo ni budi kuendelea kuwaombea ili mwenyezi mungu ili awapunguzie adhabu ya kaburi.
Ametoa rai kwa waumini wa kiisilamu ambao wamejaliwa nafasi kuendelea kuwapatia misaada mbalimbali majeruhi wa ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili na ya mkoa wa morogoro ili kuwatia moyo waweze kupona haraka.
“Waislamu tujifunze kwa tukio lililotokea mjini morogoro, ndugu zetu walitamani kula sikuuu ya Eid pamoja nasi lakini hawakuweza kutokana na ajari iliyokea, tukumbuke kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria tunapoona gari la mafuta limeanguka nasio kuwaacha wananchi wakijichotea mafuta”Alisema Haroon.
Katika hatua nyingine Haroon amewataka waumini hao kuiombea nchi amani pamoja na viongozi wake akiwemo Rais Dk John Pombe Magufuli sanjari na kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani kwa kuwatendea matendo mema ndugu jamaa na marafiki ambao wanauhitaji pamoja na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kumchukiza mwenyezi Mungu.
Ashura Hamisi na Hawa Kasimu, ni miongoni mwa waumuni wa dini ya kiislamu wamewataka vijana kuacha mara moja tabia ya kuyavamia magari ya mafuta yaliyoanguka na kujichotea mafuta ili kuweza kuepukana na vifo visivyo vya lazima na badala yake wafanye kazi halali zitakazowaingizia kipato.
Katika siku kuu ya Eid alhaj imeenda sambamba na Jumuiya hiyo ya kiislam ya Istiqmaa internation kutoa mifungo mbalimbali zaidi ya 100 kwaajili ya kuchinjwa na kugawiwa waumini na watu wengine ambao waliswali siku kuu hiyo katika Msikiti wa Alwahab uliopo katika mtaa wa nyasubi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇