Watu watatu wanaodaiwa kuwa viongozi walioanzisha maandamano ya kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nchini Afrika Kusini wamekamatwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema jeshi la polisi limeyatawanya maandamano hayo kwa kuwa hayana kibali.
“Tumewakamata wale ambao wameratibu na kuongoza maandamano hayo, Chochote ambacho wanataka kupeleka kwa umma, wanaweza kuandika barua au kutuma wawakilishi.”
Amesema Serikali ya Tanzania imepeleka watu Afrika Kusini kushughulikia suala hilo, kuwataka Watanzania kuwa watulivu, wasubiri hatua zitakazochukuliwa.
“Hili ambalo wamelifanya la kuandamana halikubaliki. Tuheshimu sheria hata pale tunapoona jambo linafanyika halipendezi lakini kuheshimu sheria ni jambo la maana sana,” amesema Mambosasa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇