Muungano wa wapinzani nchini Sudan wa 'Uhuru na Mabadiliko' umetangaza kuwa, muundo wa kipindi cha mpito nchini humo utatekelezwa katika tarehe na muda ulioainishwa.
Taarifa ya muungano huo imesisitiza kwamba, tarehe ya kuundwa serikali ya mpito nchini Sudan iko pale pale na kwamba, hakuna mabadilikko katika hilo. Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kwamba, kuundwa taasisi ya mpito nchini Sudan ni hatua ya msingi na sharti muhimu la kupatikana mwenendo wa wa amani katika nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani Omar Hassan al-Bashir.
Jumamosi ya kesho tarehe 17 Agosti pande mbilii zinatarajiwa kutia saini hati ya mwisho ya tangazo la katiba. Muswada wa tangazo hilo ulitiwa saini na pande mbili tarehe 4 mwezi huu. Aidha kwa mujibu wa makkubaliano yaliyofikkiwa kati ya muungano huo mkubwa wa upinzani nchini Sudan na Baraza la Kijeshi la Mpito, Jumapili ya keshokutwa tarehe 18 Agosti ndio siku ya kuvunjwa baraza la kijeshi linalotawala hivi sasa nchini humo.
Kwa mujibu wa mkataba huo, katika kipindi cha mpito, serikali ya kitaifa itaundwa ambapo itakuwa na jukumu la kuendesha mambo ya nchi na pia bunge jipya kubuniwa. Katika kipindi hicho cha mpito kikosi cha radiamali ya haraka kitawekwa chini ya kamandi kuu ya jeshi la Sudan.
Kwa mujibu wa mapatano ya pande mbili, kipindi cha mpito kitakuwa cha miaka mitatu na miezi mitatu ambapo Baraza la Utawala litakuwa na wanachama 6 wa kiraia na 5 wa kijeshi ambao watakuwa wakiliongoza kwa zamu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇