Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma
Serikali imesema inakuja na mkakati kabambe wa miaka mitano utakaotekelezwa na Wizara na taasisi mbalimbali katika maeneo yanayohitaji mfumo wa maboresho ya haki jinai hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga, wakati akifungua kikao cha Mawaziri, Makatibu wakuu wa Wizara na wakuu wa taasisi zinazounda jukwaa la haki jinai.
Dk. Mahiga amesema kuwa mara ya mwisho kupitia mfumo huo na kuufanyia maboresho ni takribani miaka 20 hivyo ni muhimu kwa Sasa kuupitia ili uendane na wakati uliopo.
Hata hivyo amesema kuwa baada ya mapitio ya mfumo huo yatapitishwa na kujadili maeneo yaliyopendekezwa kuboreshwa ili kufanya mfumo huo kuwa rafiki kwa wadau wote wa haki jinai.
"Niwapongeze wataalamu wetu ambao mmekua hapa kwa kwa kipindi cha miezi miwili na wote ambao mmeshiriki katika kazi hii hadi hatua hii ya leo" amesema Dkt Mahiga.
Dk .Mahiga amesema kuwa mfumo huo unahusisha mnyororo wa hatua mbalimbali zinazotolewa wakati wa kushughulikia uhalifu wa kuanzia katika ngazi ya kuzuia uhalifu kufuatilia mienendo yao wanapomaliza kutumikia adhabu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa kikao hiko ni muhimu sana kwa sababu kina lenga kufanya majadiliano ya hitimisho la mchakato wa maboresho ya sekta ndogo ya mfumo wa haki jinai.
Hata hivyo amesema kuwa ni vema nao wataalamu waliopo wanatumia nafasi hiyo kujadili maboresho hayo ili yalete tija na jamii kwa ujumla.
Naye Kamishna wa Polisi Mstaafu Laurean Tibasana, amesema kuwa wanaipongeza serikali kutokana na jitihada inazofanya katika maboresho ya sekta ndogo ya sheria ya mfumo wa haki jinai.
Aidha amesema kuwa hilo litasaidia nchi kuwa na maendeleo kutokana na kwamba kutasaidia kupunguza uhalifu mbalimbali ikiwemo kurekebisha tabia za wahalifu na kufuatilia mienendo yao wanapokuwa wamemaliza kutumikia adhabu walizopewa.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇