Katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwishoni mwaka huu, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma wametakiwa kudumisha amani na utulivu wakati huu wa maandalizi ili muda ukifika ufanyike kwa amani na utulivu.
Wito huo umetolewa na Ofisa wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Emmanuel Kuboja, wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika wilayani hapo.
Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Kuboja amesema mahali penye utulivu hata maendeleo huwa makubwa na kuwataka madiwani katika halmashauri hiyo kuendelea kuwa watulivu na kudumisha amani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Danford Chisomi, alisema, halmashauri hiyo itaendelea kutoa mchango katika kila kata hasa ukamilishaji maboma na kuendeleza, kukuza na kusimamia miradi ya maendeleo.
Alisema hayo alipokuwa akijibu baadhi ya changamoto zilizotolewa na baadhi ya madiwani hasa katika ujenzi wa maboma na madarasa katika kata mbalimbali.
"Ni lazima kwa viongozi wa halmashauri kuungana ili kuongeza nguvu ya kusimamia miradi mbalimbali, " alisema.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇