Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemuagiza mkuu wa jeshi la polisi mkoani Kagera kufanya msako mkali wa kuwabaini wananchi katika eneo la Benako wilayani Ngara mkoani hapa waliohusika katika zoezi la kuchota mafuta au kujaribu kuchota mafuta kwenye lori la mafuta lililopata ajali jana asbuhi, August 25 2019,
Akionyesha kusikitishwa na tukio hilo Mkuu wa mkoa Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa hakika ni hali ya kusitajabisha na kuuzunisha kutokana na tukio hilo lililowahusisha wanawake , wanaume na watoto walioonekana katika clip ya video inayotembea kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii ikionyesha baadhi ya wananchi katika eneo la Benako wilayani Ngara mkoani hapa wakichota mafuta k kwenye lori la mafuta lililopata ajali August 25 2019.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema video hiyo inayowaonyesha wananchi hao wakichota mafuta na kusema kuwa waliohusika katika ni wanawake, wanaume na watoto walionekana na vidumu pamoja na Ndoo.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imelihusisha gari aina Fuso, lenye namba za usajili 456 CMI lililokuwa likiendeshwa na mtu mwenye asili ya Kiarabu na kuwa amepelekwa katika hospitali iliyopo wilayani humo ili kupatiwa matibabu.
Kufuatia hali hiyo Brigedia Marco Gaguti amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanya msako mkali katika maeneo ya vijiji jirani na kuhakikisha wahusika waliojaribu wa walochota mafuta wanatiwa nguvuni.
‘’Hali hii inadhihilisha kwamba kuna baadhi ya wananchi hawajajifunza au hawataki kujifunza kutokana na ajali iliyotokea August 10 mwaka huu huko mkoani Morogoro hivyo basi Naagiza Wahusika hao wakamatwe mara moja ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Aidha mkuu wa mkoa ametumia fulsa hiyo kutoa onyo kwa wanakagera na watanzania wote kwa ujumla kutambua kuwa ni vyema kujiepusha na Matukio ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa katika taifa hili.
Amesema kuwa Mkoa wa Kagera unazo njia za kwenda nchi jirani za Rwanda , Burundi, na Uganda na kumekuwa na magari mengi na makubwa ya bidhaa mbali mbali ikiwemo mafuta na Magari hayo hutumia njia hizo hivyo ni vyema kujiepusha na matukio yoyote yale ambayo kwa njia moja ama nyingine yanayoweza kuleta madhara na kuleta vilio katika taifa la tanzanzania
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇