Rais wa Zambia Mh. Edgar Changwa Lungu,ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) pichani kati akiongoza kikao cha ulinzi na usalama kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC (SADC) kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika – SADC, Dkt Stergomena Tax.
Rais wa Angola Mh. Joao Lourenco Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) anayemaliza muda wake akiwa katika kikao hicho kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zimbabwe Mh. Emmerson Dambudzo Mnangagwa anayechukua nafasi ya Uenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) akipitia baadhi ya nyaraka za kikao hicho kilichofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇