Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amemtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ya Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 15,2019.
Rais Ramaphosa ameongozana na mke wake, Dk Tshepo Motsepe ambao wamepokelewa na mwenyeji wao, Rais Magufuli na mkewe, Janeth katika viwanja vya Ikulu.
Mara baada ya kuwasili, Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amepata heshima ya kupigiwa wimbo wa taifa na mizinga pamoja na kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇