LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 18, 2019

MKUTANO WA SADC WAHITIMISHWA, RAIS MAGUFULI ATAJA MAMBO WALIYOKUBALIANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa SADC, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa wamekubaliana mambo kadhaa katika kikao cha wakuu wa nchi 16 kilichofanyika jana jioni Ikulu jijini Dar es salaam yakiwamo suala la kuondolewa kwa vikwazo kwa Zimbabwe, kufuatilia hali ya usalama nchini Congo na ombi la Burundikujiunga na jumuiya hiyo.

Mengine ni kuwekeza kwenye miundombinu itakayowezesha kukua kwa uchumi katika ukanda wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, kuwa na chombo cha kukabiliana na majnga na suala la upatikanaji wa mapato.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano huo wa SADC wa siku mbili uliomalizika leo Jumapili Agosti 18, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hotuba ya kuhitimisha mkutano huo, Rais Dk. John Magufuli amesema wakuu wa nchi wamekubaliana kuendelea kufuatilia hali ya usalama nchini Congo lakini pia wameiagiza sekretarieti kuharakisha chombo cha kukabiliana na majanga kitakachosaidia nchi wanachama kukabiliana na majanga kama vile njaa, mafuriko, vimbunga, magonjwa ya mlipuko na mengineyo.

Amesema katika mkutano huo pia, wakuu wa nchi walipitia hali ya uchumi katika ukanda wao ambapo uchumi wa nchi hizo ulishindwa kukua kama ulivyotarajiwa kwa asilimia saba na kushuka hadi asilimia 3.1, hivyo wamekubaliana kuwekeza kwenye miundombinu kwa kuwa ni mojawapo ya kikwazo cha kukua kwa uchumi kwenye bara la Afrika ikiwamo nchi za SADC.

Pamoja na mambo mengine, amesema mkutano huo pia umepitisha mpango wa kuongeza mapato kwa SADC ambapo nchi wanachama zitakuwa na hiyari ya kuchagua njia bora ya kuchangia.

1 comment:

  1. Kweli nimefarijika Sana na huu mkutano wa viongizi.wetu,natoa pongezi zangu,Kwa maoni yangu Kwa uongozi was doctor,tutasogea ki maendekeo.big up magufuli piga KAZI 😀😁

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages