Kundi la waasi la Houthi la Yemen limesema lilirusha makombora 10 dhidi ya uwanja wa ndege wa Jizan nchini Saudi Arabia jana usiku.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa kituo cha televisheni cha al-Masirah kinachomilikiwa na kundi hilo imemnukuu msemaji wa jeshi la waasi hao Yahya Sarea akisema, makombora 10 aina ya Badr-1 yamerushwa kwa pamoja dhidi ya uwanja wa ndege wa Jizan, na yamelenga ndege za kijeshi na helikopta za kivita aina ya Apache ndani ya uwanja huo, na kwamba askari kadhaa wa Saudia wameuawa kwenye shambulizi hilo.
Pia amesema, jeshi la Houthi litafanya mashambulizi mengi zaidi katika kipindi kijacho
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇