LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2019

JOE BIDEN: UBAGUZI WA RANGI UMEKITA MIZIZI NCHINI MAREKANI KATIKA UTAWALA WA TRUMP

Joe Biden ambaye anatazamiwa kuwania nafasi ya kuchuana na Trump katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani amesema kuwa, ubaguzi wa rangi ni tatizo lililokita mizizi nchini Marekani na unahusishwa na wazaungu.
Biden ameongeza kuwa: "Ubaguzi umekuwapo Marekani kwa miaka mingi na makundi kadhaa nchini humo yanaamini kwamba, watu weupe ndio kizazi bora zaidi, lakini matamshi yanayotolewa na Rais Doland Trump yamezidisha tatizo hilo."
Joe Biden
Tatizo la ubaguzi hususan dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika limekuwa mjadala mkubwa nchini Marekani tangu baada ya shambulizi lililofanyika mwezi uliopita wa Julai katika mji wa El Paso jimboni Texas na kuua watu wasiopungua 20. Katika hujuma hiyo Patrick Crusius ambaye ana misimamo ya ubaguzi wa rangi alivamia eneo la maduka la Walmart na kuwafyatulia risasi na kuwaua watu 22 na kuwajeruhi wengine 24.
Kijana huyo ambaye ni muungaji mkono wa sera za ubaguzi wa rangi za Rais wa Marekani Donald Trump, alisema amefanya mauaji hayo kupinga umiminikaji wa wahamiaji katika jimbo hilo wanaotoka nchini Mexico.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages