LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 27, 2019

IRAN ISHAMFAHAMISHA MACRON HAIFANYI MAZUNGUMZO KUHUSU MAKOMBORA

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelikataa pendekezo la Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa la kuweka kadhia ya makombora ya kujihami ya Iran katika ajenda ya mazungumzo mapya.
Duru zimeidokezea Televisheni ya Press TV kuwa, Iran tayari imeshatoa jibu kwa pendekezo la Macron na kumfahamisha kuwa haikubali kufanya mazungumzo kuhusu mpango wake wa makombora ya kujihami.
Akizungumza na Press TV, afisa ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa Iran pia imekataa pendekezo la Ufaransa la kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya eneo la Asia Magharibi na uwepo wa Iran katika eneo hilo.
Kuhusu pendekezo la rais wa Ufaransa la kuanzisha mfuko wa dola bilioni 15 kwa lengo la kuiwezesha Iran kufanya biashara, afisa huyo ameiambia Press TV kuwa Iran imesema inaweza kutafakiri kuhusu kubatilisha uamuzi wake wa kuacha kutekeleza baadhi ya vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA iwapo mfuko huo utaanzishwa.
Waziri Zarif (aliyekunja mikono) katika mazungumzo na Rais Macron wa Ufaransa (wa pili kulia) pembeni ya kikao cha G7
Kuhusu uwezekano wa mazungumzo baina ya Rais Hassan Rouhani wa Iran na Rais Donald Trump wa Marekani, afisa hiyo amedokeza kuwa, Iran imeshatangaza kuwa, sharti la mazungumzo yoyote na Marekani ni Washington kurejea katika mapatano ya nyuklia ambayo yanajulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.
Aidha afisa hiyo amedokeza kuwa, Iran haitashiriki katika mazungumzo maadamu vikwazo havijaondolewa na maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu kuzingatiwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages