LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 8, 2019

DKT SHEIN: NCHI ZA SADC TUTOE KIPAUMBELE KWA BIDHAA

 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia  Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini  mwa Afrika SADC, (hawapo pichani), kuhusu maonesho yaViwanda  alipokuwa akifunga maonesho hayo  leo 08 Agosti, 2019  Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kuhusu bidhaa za kampuni hiyo  kwenye Maonesho ya Wiki ya Viwanda, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, alipokuwa akitembelea na kufunga Maonesho hayo leo 08 Agosti, 2019  
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kiwanda cha viatu cha  gereza  la Karanga (Moshi), kuhusu bidhaa zinazotengenezwa kwa ngozi, kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Paramagamba Kabudi, maonesho hayo yamefungwa rasmi leo 08 Agosti, 2019. 
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akitoa neno la Shukurani kwa Washiriki wa Wiki ya Viwanda kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, (hawapo pichani), Kuhusu maonesho ya Viwanda  yaliyofungwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein. 
 Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale  wa Serikali ya Zanzibar akizungumza na Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, kuhusu kutembelea viwanda na vivutio vya utalii vilivyoko Zanzibar, Maonesho hayo  yalifungwa rasmi leo na Rais Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wa tatu kutoka  kushoto waliokaa). 
 : Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya Pamoja  na  Viongozi (SADC) na Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,  kwenye  hafla ya kufunga maoneshoa ya wiki ya viwanda. 

   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya Pamoja  na  Viongozi (SADC) na Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,  kwenye  hafla ya kufunga maoneshoa ya wiki ya viwanda.



Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuweka mkazo wa matumizi ya bidhaa zake  na wataalamu wake wa ndani katika kutengeneza fursa za ajira na masoko ndani ya ukanda huo ili kukuza sekta za viwanda na biashara ndani ya jumuiya hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Maadhimisho na Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda katika Nchi za SADC leo Alhamisi (Agosti 8, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Shein alisema umefika wakati kwa mataifa hayo kuzalisha bidhaa bora zenye kuweza kuleta ushindani katika masoko ya ndani na nje ya Jumuiya hiyo.
Dkt. Shein alisema Mataifa ya SADC hayana budi kutumia fursa ya maonesho hayo katika kutangaza fursa za ujuzi na ubunifu  kwa kuzalisha na kutengeneza mtandao wa imara wa mawasiliano baina ya Nchi hizo na kuweza kuwa na soko la pamoja litakalowawezesha kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wa Mataifa hayo.
Kwa mujibu wa Dkt. Shein aliongeza kuwa ili kufikia malengo ya uzalishaji wa bidhaa bora za viwandani ni wajibu wa Serikali zote kutengeneza mtandao imara wa miundombonu ikiwemo matumizi ya tekonolojia ya habari na mawasiliano kwa kuunda mikakati ya pamoja ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Jumuiya hiyo uliolenga katika kuimarisha sekta ya viwanda ndani ya jumuiya hiyo.
“Hatujakataa mchango wa wataalamu na bidhaa za nje, lakini chako ni chako na mwenzako si chako, hivyo hakikunyima usikasirike, ni wakati wetu sasa kuweka mkazo katika kutegemea wataalamu wetu na teknolojia zetu katika uzalishaji wa bidhaa zetu” alisema Dkt. Shein.
Aliongeza kuwa Nchi za Jumuiya hiyo hazina budi kutumia fursa za Maonesho na midahalo mbalimbali ya wataalamu inayojadiliwa katika Mikutano ya Jumuiya hiyo ili kuweza kubaini changamoto na hatua mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa ili kuiwezesha jumuiya hiyo kupiga hatua kubwa za Maendeleo ikiwemo kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wake.
Akifafanua zaidi Dkt. Shein aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali katika uboreshaji wa miundombinu ya miradi ya Maendeleo ambayo imekuwa kichocheo kikubwa cha fursa za ajira kwa vijana sambamba na kutengeneza mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kushiriki katika uchumi wa viwanda.
Akitolea mfano, Dkt. Shein alitaja baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa viwanda  vikubwa, vya kati na vidogo ambavyo kwa pamoja vinaifanya Tanzania kuwa 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages