Meya wa Mogadishu mji mkuu wa Somalia jana alijeruhiwa na watu wengine sita kuaga dunia katika mlipuko wa bomu la kujilipua uliotekelezwa jana katika jengo moja la serikali. Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari wa Somalia.
Mohamed Abdi Hayir Waziri wa Habari wa Somalia amesema kuwa Meya Abdirahman Omar Osman amejeruhiwa vibaya katika mlipuko huo. Makamishna wawili wa wilaya na wakurugenzi watatu wa mikoa pia ni miongoni mwa watu waliouliwa katika mlipuko huo wa Mogadishu. Kundi la kigaidi la al Shabaab lenye makao yake huko Somalia limedai kuhusika na shambulio hilo la bomu la kujilipua na kusema kuwa shambulio hilo lilikusudiwa kuwalenga maafisa wa Umoja wa Mataifa ambao walikuwa wakilizuru jengo hilo la serikali.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇