Duru zenye mfungamano na wanamgambo wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya wanaoongozwa na kamanda Khalifa Haftar zimeripoti kuwa wanamgambo hao wametungua droni ya Uturuki katika anga ya mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Wanamgambo hao wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya wanaoongozwa na jenerali Khalifa Haftar wamesema kuwa ndege hiyo isiyo na rubani wameitunguwa katika eneo la Ain Zara huko Tripoli. Katika upande mwingine, duru moja ya kijeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imeripoti habari ya kuuawa wanamgambo wanane wa Khalifa Haftar katika mashambulizi ya anga ya Uturuki. Kabla ya hapo, wanamgambo hao wa Khalifa Haftar walitangaza kuwa wamejiandaa kufanya shambulio kubwa katika mji mkuu Tripoli na kuwataka wakazi wa mji mkuu huo wajiandae kwa mashambulio makali kwa ajili ya kuidhibiti Tripoli.
Wanamgambo hao wanaoongozwa na Kamanda Haftar walianza kutekeleza mashambulio huko Tripoli tangu tarehe Nne Apriki mwaka huu na hadi kufikia sasa vimeshindwa kuudhibiti mji mkuu huo wa Libya. Hayo yanajiri katika hali ambayo Baraza la Uongozi la Serikali ya Mapatano ya Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa kwa mujibu wa ripoti na taarifa zilizopo, Ufaransa, Misri na Imarati zinajiandaa kushiriki kwenye mashambulio makubwa yaliyopangwa kufanywa hivi karibuni na vikosi vya Haftar dhidi ya mji mkuu Tripoli.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇