LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 1, 2019

TAWODEF YATOA ELIMU YA UJASILIAMALI KWA JUKWAA LA WANAWAKE.


 Viongozi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Misugusugu iliyopo Wilaya ya Kibaha wakisikiliza Maelekezo ya Utengenezaji wa Batiki na Sabuni ya Maji na Vipande kutoka kwa Afisa wa Taasisi ya Tawodef.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Misugusugu, Sauda Mpambalyoto (katikati) akizungumza wakati wa kuwakaribisha wakufunzi kutoka Taasisi ya Tawodef Kuwafundisha Ujasiliamali wa Utengenezaji wa Batiki na Sabuni ya Maji na Sabuni. Kushoto Kwake ni Katibu wa Uwt Kibaha Mjini,Proscovia Mwambi na Katibu Ofisi ya Mbunge Jimbo la Kibaha Mjini, Method Mselewa.
Katibu wa Ofisi ya Jimbo la Kibaha Mjini, Method Mselewa (katikati) akiangalia mojawapo ya kitenge cha batiki ambacho kimetengenezwa na taasisi ya Tawodef.

NA:ELISA SHUNDA,KIBAHA.
TAASISI Isiyo ya Kiserikali Inayoshughulika na Maendeleo ya Jamii na Wanawake Nchini (TAWODEF) Imetoa Elimu ya Ujasiliamali wa Utengenezaji wa Sabuni za Miche, Maji na Batiki kwa Wakinamama wa Jukwaa la Wanawake la Misugusugu kwa Ajili ya Kuwawezesha Kiuchumi.



Akizungumza Kuhusu Utoaji wa Elimu ya Ujasiliamali kwa Kikundi hicho Wilayani Kibaha Leo, Mratibu wa Taasisi hiyo, Fabiana Salvatory, Alisema Kuwa Wamekuja katika Kata ya Misugusugu Kutoa Elimu ya Ujasiliamali katika Utengenezaji wa Batiki Zenye Viwango na Sabuni za Maji na Vipande kwa Wanawake Hao ili Kukuza Uchumi kwa Familia na Jamii Kwa Ujumla kwa Kuwa Ukimfundisha Mwanamke Umeiwezesha Jamii Nzima.

''Sisi Tawodef Tupo Hapa Misugusugu katika Kumuwezesha Mwanamke Aweze Kupiga Hatua Kimaendeleo na Kiuchumi kwa Kuwa Tunaamini Ukimuwezesha Mwanamke Umeisaidia Jamii Nzima Inayomzunguka Lakini Pia Tunatoa Elimu Juu ya Mikopo Wanayoomba Ili Waipatapo Wajue Nini cha Kufanya Ili Muda wa Marejesho Ukifika Isiwagharimu Bali Walipe na Biashara Zao Zidumu na Maisha YAo Yaendelee Kama Kawaida Isiwe Mkopo Umfanye Mwanamke Huyo Ateseke na Awe na Msongo wa Mawazo Juu ya Urudishaji Wa Fedha Alizokopa.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Misugusugu,Sauda Mpambalyoto, Ameishukuru Taasisi ya Tawodef Kupitia Mkurugenzi Wake,Mh.Celina Koka kwa Kuweza Kuwapatia Elimu Hiyo ya Ujasiliamali na Kuiomba Taasisi Hiyo Isiishie kwa Kata Hiyo Iende katika Kata Zingine 14 za Kibaha Mjini Kutoa Elimu Hiyo ya Ujasiliamali.

''Tunamshukuru Sana Mke wa Mbunge Wetu wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mama Celina Koka Kupitia Taasisi Yake ya Tawodef kwa Kuweza Kutusaidia Siku ya Leo Sisi Wakinamama wa Kata ya Misugusugu Kupata Elimu Hii ya Ujasiliamali Namuomba Asiishie na Sisi Tu Aendelee na Taasisi Yake Kuwapatia Wanawake Wote wa jimbo Zima la Kibaha Mjini na Sehemu Zingine kwa Jinsi Atakavyoweza Kupitia Taasisi Yake'' Alisema Mwenyekiti Mpambalyoto.

Kwa Upande Wake Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Proscovia Mwambi, Ameipongeza Taasisi Hiyo kwa Kufanya Mafunzo Hayo kwa Wanawake na Kuwasihi Wakinamama Kutoka Sehemu Mbalimbali na Vyama Mbalimbali Kushirikiana na Jukwaa la Wanawake la Kata ya Misugusugu kwa Kuwa Jukwaa Hilo Si la CCM Bali ni La Wanawake Wapenda Maendeleo wa Kata Hiyo.

Kwa Niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,Slyvestor Koka, Method Mselewa Alisema Kuwa Ofisi ya Mbunge Inaungana na Taasisi Hiyo katika Kuwainua Wanawake Kiuchumi na Amewahakikishia Kupitia Ofisi Hiyo Itajitahidi Kila Liwezekanalo Kila Mradi Unaofika katika Halmashauri ya Kibaha Mjini Unaowahusu Wanawake Ofisi Hiyo Itasimama Kidete Kuhakikisha Wanawake wa Jimbo Hilo Wananufaika Nalo.
Mwishoo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages