LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2019

RAIA 300 WA MISRI WAZUIWA KUFANYA HIJJA SAUDIA

Saudia imewazuia raia 300 kutoka Misri waliokuwa na viza ya kitalii na nia ya kwenda kwenye ardhi takatifu kuhiji.

Kwa mujibu wa habari kutoka katika gazeti la Misri Ahbar el-Yevm, Wamisri hao 300 waliokuwa wakienda kufanya hija wamerudishwa nchini kabla hawajatimiza lengo lao.

Katika taarifa ya maandishi kutoka wizara ya mambo ya nje ya Misri ikizungumzia kadhia hiyo ilisema haitaruhusu tena watu wanaopatiwa viza za kitalii na ziara kupitia  mashirika yanayojihusisha na hijja kutoka Misri, watakaoruhusiwa ni wale tu waliokuwa na viza maalumu za hijja.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages