Maafisa nchini Pakistan leo wamemkamata Hafiz Saeed, mtuhumiwa wa shambulizi la siku nne katika mji wa Mumbai nchini India mwaka wa 2008, akikabiliwa na mashitaka ya kufadhili ugaidi.Hatua hiyo imekuja siku chache kabla ya ziara ya Waziri Mkuu Imran wa Pakistan Khan mjini Washington, ambaye ameapa kuyaangamiza makundi ya wanamgambo wa itikadi kali yanayoendesha harakati zao nchini Pakistan.
Saeed, ambaye yuko kwenye orodha ya Marekani ya magaidi wanaosakwa, ni muasisi wa Lashkar-e-Taiba, kundi la wanamgambo linalolaumiwa na Marekani na India kwa kufanya mashambulizi ya Mumbai, ambayo yaliwauwa zaidi ya watu 160.
Anakanusha kuhusika kwa vyovyote na shambulizi hilo akisema mtandao wake, ambao una seminari 300 na shule, hospitali, kampuni ya uchapishaji na huduma za dharura kwa wagonjwa, hauna mahusiano na makundi ya wanamgambo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇