Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Sara Msafiri, siku ya Alhamisi
11, Julai 2019, ameipongeza benki ya UBA Tanzania kwa mchango mkubwa
ambao benki hiyo inatoa kwenye sekta ya elimu kwa kutoa vitabu Zaidi ya
15000 kwa shule za sekondari zote zenye uhitaji wa vitabu zilizopo
wilaya ya Kigamboni.
UBA TANZANIA kupitia UBA Foundation chini ya mpango wa ‘Read Africa
Initiative’ imetoa vitabu hivyo takribani 1500 vya fasihi kwenye shule
za serikali zilizopo wilaya mpya ya Kigamboni, shule ambazo Bank ya UBA
Tanzania imetembelea ni Nguva Sekondari, Aboudjumbe sekondari na
Pembamnazi sekondari zote zipo ndani ya wilaya hiyo.Wengine waliokuwepo kwenye tukio hilo ni Mkurugenzi wa wilaya Arch Ng’wilabuzu Ludigija na afisa elimu wa wilaya, ambapo uongozi wa benki hiyo ukiongozwa na ndugu Geofrey Mtawa ambaye ni mkuu wa kitengo cha biashara ndogondogo na za kati (UBA Head of Retail and MSME banking), Mkuu wa kitengo cha dijitali bwana Asupya Nalingigwa, Afisa mawasiliano Anitha Pallangyo na Msimamizi wa tovuti ya benki bwana Kassim Riyami.
“Vitabu hivi vilivyotolewa na benki ya UBA Tanzania, vitasaidia katika kuwajengea vijana wetu kupenda kujisomea na kujiwekea utaratibu wa kujisomea mara kwa mara, pamoja na kuwaongezea uwezo katika masomo yao,” alisema Mheshimiwa Msafiri wakati wa ziara hiyo.
Ndugu Geofrey alieleza kuwa vitabu hivyo ni vya hadhi ya juu Africa, ambavyo vimeboreshwa Zaidi ili kuwawezesha wanafunzi na walimu kuvielewa kwa lugha rahisi na yenye kuelimisha. Mheshimiwa Msafiri alisisitiza kuwa vitabu hivyo vitasaidia kuongeza idadi ya vitabu vyenye ubora kwenye maktaba za shule husika.
Mbali na kutoa vitabu hivyo, UBA Tanzania imekua ikisaidia sekta ya elimu kwa kutoa vitabu kwenye shule mbalimbali ikiwa ni pamoja na wilaya zaa ilala, temeke, kisarawe na Pwani, pamoja na kutoa elimu ya ujasiriamali bure kwa vijana na wanawake kupitia mpango wao wa ‘Each one teach one’.
Baadhi ya vitabu vilivyotolewa na benki hiyo ni vile vinavyotumika kwenye mitaala ya Tanzania kama Things Fall Apart, The Girl That Can, The Fisherman, na vinginevyo vingi kutoka kwa waandishi mashuhuri kutoka Nigeria na hutumika kwenye mitaala ya shule mbalimbali Africa.
Mtawa, ambae alimuwakilisha mkurugenzi wa benki ya UBA alisema UBA inafurahi kuongoza usukani kwenye kuwajengea vijana hususani wa shule za sekondari tabia ya kujisomea, kupitia mpango wake wa Read Africa Initiative. Alisisitiza kuwa elimu ni miongoni mwa maeneo makuu matatu ambayo benki ya UBA imejikita kusaidia katika Afrika kama moja ya njia ya kurudisha kwa jamii ambao ni wadau wakubwa wa benki, maeneo mengine yakiwa ni afya na mazingira.
UBA Tanzania ambayo makao makuu yake yapo barabara ya Nyerere jirani na daraja la Mfugale (Tazara Flyover), ni kampuni tanzu ya UBA Group moja kati ya benki zinazoongoza duniani, iliyopo kwenye nchi Zaidi ya 20 Africa na kwenye vituo vikubwa vya biashara New York, Paris na London uingereza. Inatoa huduma za kawaida za kibenki, pamoja na za kidijitali na imetunukiwa tuzo ya kuwa benki bora na inayoongoza kidijitali Afrika kwa mwaka 2018 ambazo hutolewa na Euromoney.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri(wa nne kushoto), Katibu tawala wa wilaya hiyo Rahel Mhando(wapili kushoto),Mkuu wa kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa UBA Geofrey Mtawa(wa tatu kushoto)Afisa Uhusiano wa UBA,Anitha Pallango(wanne kulia) pamoja na Maofisa wengine wa Serikali wilayani Kigamboni,Afisa Elimu Sekondari Jumanne Mwakalinga, Kaimu Mkurugenzi Charles Lawiso, Mchumi Maxmillian Manyuka na Mkuu wa Idara ya Mipango ndugu Mosses Chillah,wakiwa katika picha ya pamoja katika tukio la ugawaji wa vitabu wilayani kigamboni.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Ndogondogo na za Kati wa UBA Tanzania Geofrey Mtawa,akiwa na wanafunzi katika tukio la ugawaji vitabu
Wanafunzi wa Wilaya ya Kigamboni wakimsikiliza Geofrey Mtawa ambae ni mkuu wa kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa UBA
Wanafunzi wakiwa wameshika Vitabu walivyogawiwa na UBA Tanzania wilayani Kigamboni
Mkuu wa kitengo cha biashara ndogondogo na za kati Geofrey Mtawa na Afisa mahusiano wa UBA Tanaznia Anitha Pallango wakisoma vitabu katika tukio la ugawaji vitabu hivyo
Wanafunzi wakiwa mamesisimama kwa furaha huku wakisubiri kugawiwa vitabu vilivyotolewa na UBA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇