LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2019

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI YA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA SADC.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert  Ibuge akiwasilisha mada wakati wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na  kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini  Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa kundi la pili la waandishi hao.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na  kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo .
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Zamaradi Kawawa akizungumza  wakati wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini  Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa  waandishi hao. 
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika  na kuripoti habari za SADC kwa weledi Henry Mabumo  akieleza  jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na Jumuiya hiyo kupitia fursa zilizopo katika nchi wanachama, hayo yamejiri leo Julai 12, 2019 mjini Morogoro wakati wa siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi hao.  
Katibu Mkuu mstaafu Balozi Hebert Mrango akisisitiza jambo  wakati wa mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, hayo yamejiri mjini Morogoro Julai 12, 2019 ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa waandishi hao  yanafanyika kwa siku tatu.
Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu  Mussa Uledi akijibu hoja mbalimbali za waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika  (SADC) yanayoendelea mjini  Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo. Picha zote na Abukari Kafumba- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages