LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 11, 2019

MANGULA AKUTANA NA MAKAMU WAZIRI MKUU WA VIETNAM, LEO

CCM Lumumba, Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Vietnam, ukiongozwa na Makamu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Trinh Dinh Dung, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, walijikita zaidi katika mahusiano baina ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam na Serikali zinazooongozwa na vyama hivyo.

"Kwa kweli Sisi CCM na Serikali yake tunaridhirika na kufurahia sana jinsi Chama Cha Kimomunisti na Serikali yake ya Vietnam vinavyotupa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo", alisema Mangula.

Kwa Upande wake Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam alisema, nchi hiyo nayo inaridhika na mshikamano uliopo kati ya nchi hiyo na Tanzania na kuomba ushirikiano na mshikamano huo udumu.

Vyama vya Kikomunusti cha Vietnam na CCM cha Tanzania ni vyama marafiki wa siku nyingi. HABARI PICHA ZA TUKIO/>BOFYA HAPA


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages