Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu CCM, Pius Msekwa amesema malalamiko ya makatibu wakuu wawili wa chama hicho atayapeleka ngazi za juu kwa hatua zaidi.
Juzi, makatibu wakuu hao wawili wastaafu wa CCM, Yusuf Makambana Abdulrahman Kinana, walimwandikia barua Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.
Msekwa ambaye alisema barua hiyo ambayo ni ya kwanza kuwafikia wao kama Baraza la Wazee Wastaafu, kwa kawaida itapelekwa kwenye chama hicho ambacho ndicho kinachopaswa kuitisha vikao kushughulikia malalamiko yaliyotajwa.
Amesema nakala nyingine za barua hiyo zimepelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.
“Hii ni mara ya kwanza kupokea malalamiko ya aina hii, kwanza hakuna utaratibu wa kawaida, lakini tutafuata taratibu za chama, tutapeleka kwenye chama chenyewe." Amesema na kuongeza;
“Barua hii nakala yake imeenda pia kwa Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu"
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇