LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 19, 2019

IRGC: HIVI KARIBUNI TUTAONYESHA PICHA ZA MELI YA MAREKANI ILI KUFICHUA UONGO WA TRUMP

Ofisi hiyo ya jeshi la SEPAH imesema kuwa, hivi karibuni itaanika picha zilizochukuliwa na ndege ya kikosi cha anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kutoka kwenye meli ya kivita ya Marekani ya USS Boxer. Hii ni katika hali ambayo siku ya Alkhamisi Rais Donald Trump wa Marekani alidai kwamba, meli ya kivita ya nchi yake aina ya USS Boxer iliiangusha ndege isiyo na rubani ya Iran baada ya ndege hiyo eti kuikaribia meli hiyo.
Madai hayo yalitolewa katika hali ambayo katika taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) haikutaja kwa namna yoyote iwapo ndege hiyo inayodaiwa kuangushwa ni mali ya Iran au la.
Meli ya kivita ya USS Boxer ya Marekani inayodaiwa kutungua ndege ya Iran, ilhali ni uongo mtupu
Aidha taarifa hiyo imeongeza kwamba picha hizo zitaonyesha kwamba kabla ya meli ya kivita ya Marekani kufika eneo la Lango Bahari la Hormoz, ndege hiyo isiyo na rubani ya Iran ilikuwa ikitekeleza majukumu yake katika eneo hilo na imesisitiza kuwa, ndege hiyo iliweza kurudi salama katika kambi ya jeshi bila kutunguliwa.
Leo Ofisi Kuu ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) imesisitiza kwamba, kuchapishwa picha za ndege hiyo isiyo na rubani zilizochukuliwa kwenye meli ya kivita ya Marekani ya USS Boxer, kutaweka wazi madai ya uongo ya rais wa Marekani mbele ya walimwengu.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages