LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2019

BRITSH AIRWAYS YAANZA TENA SAFRI ZA MISRI

Shirika la ndege la Uingereza, British Airways, limesema leo kuwa litarejesha safari zake kuelekea nchini Misiri baada ya kuzisitisha kwa muda wa wiki moja kutokana na hali ya kiusalama.Kupitia ujumbe wa barua pepe, msemaji wa shirika hilo amesema kuwa baada ya tathmini ya kina ya mipango ya kiusalama, shirika hilo limeridhika na kwamba huduma zake zitaanza tena hii leo.

Shirika hilo la ndege lilikuwa limesitisha safari za kuelekea Cairo siku ya Jumamosi kwa siku saba kama mbinu ya tahadhari ya kiusalama.Mkuu wa shirika la ndege la serikali ya Misri, EgyptAir, awali alisema kuwa uamuzi wa British Airways haukuwa na sababu za maana, huku Waziri wa Usafiri wa Anga, Younis Al-Masry, akielezea kutoridhika kwake na uamuzi huo.

Siku ya Jumapili, wizara ya usafiri wa anga ya Misri ilisema kuwa shirika la British Airways lilichukuwa hatua hiyo bila kushauriana na maafisa wa serikali wa Misri.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages