LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 18, 2019

BALOZI SEIF KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA MZANZIBAR

Na Thabit Hamidu, Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif  Ali Iddi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 24 la utamaduni wa mzanzibar ambalo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Mapinduzi square (Kisonge) kuanzia tarehe 19 mpaka 25 Julai.

Hayo ameyasema Waziri wa Vijana,Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Ali Amani Karume wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya tamasha la 24 la mzanzibar.

Amesema  kuwa Tamasha la utamaduni wa Mzanzibar ni sehemu muhimu ya kukuza na kuendeleza Sanaa hapa nchini hivyo ni vyema kulinda na kukuza utamaduni huo kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Aidha amesema  kuwa tamasha hilo liliasisiwa mwaka 1995 na aliokuwa Raisi wa awamu ya nne Dkt.Salmin Amuor Juma pale alipotamka kwamba kila mwaka Wazanzibar wawe na wiki ya kuadhimisha utamaduni wao.

Balozi Karume aliwataka vijana kuendelea kuenzi na kulinda tamaduni ili kuweza kujifunza na kupata mwamko juu ya kutambua umuhimu wa kuutuiana kukuza Sanaa kwa maendeleo.

Hata hivyo aliwataka wananchi kujumuika pamoja katika maonesho mbalimbali ya tamasha hilo ili kufurahia Sanaa na urithi wa utamaduni ili kuendelea kulinda tamaduni zao.

Kauli mbiu ya Tamasha hilo ni “Utamaduni ni ngao kwa ustawi wa jamii yetu

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages