LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2019

ASILIMIA 59 YA WAMAREKANI WANAPINGA JUMBE ZA KIBAGUZI ZA TRUMP

Kwa mujibu wa uchunguzi huo mpya wa maoni uliofanywa na kanali ya televisheni ya CBS ya nchini Marekani na taasisi ya uchunguzi wa maoni ya kimataifa ya YouGov ya nchini Uingereza, asilimia 59 ya Wamarekani wamepinga matamshi ya wiki iliyopita ya Donald Trump kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter dhidi ya wabunge wanne wasio wazungu wa chama cha Democrat nchini Marekani. Matokeo hayo ambayo dondoo zake zimetangazwa kikamilifu na kanali hiyo ya televisheni ya Marekani, yametolewa katika hali ambayo kati ya kila raia 10 wa Marekani, tisa kati yao wanaamini kwamba masuala ya ubaguzi wa rangi yatazusha mpasuko nchini.
Raia wa Marekani hawamtaki Trump mbaguzi awaongoze
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, ndani ya Wademocrat pia kuna idadi kubwa ya watu wanaopinga ubaguzi wa rangi wa rais huyo na wametangaza upinzani wao kwa kiwango cha asilimia 88. Katika siku chache zilizopita rais wa Marekani, Donald Trump alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, akiwashambulia vikali kwa maneno ya ubaguzi wa rangi wabunge wanne wasio wazungu ambao ni wanawake wanaojulikana kwa majina ya Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib. Hata hivyo na licha ya maneno yake hayo yenye chuki na udhalilisha kulalamikiwa vikali, lakini rais huyo bado anaendelea kuwashambulia kibaguzi wanawake hao wa chama cha Democrat.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages