LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 3, 2019

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AHUDHURIA HAFLA YA UZINDUZI WA BARAZA JIPYA LA TAIFA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa baraza hilo kushirikiana na Serikali wakati akizindua Baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Stella Ikupa akielezea jambo kwa wajumbe wa Baraza wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika tarehe 2 Juni, 2019 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija akitoa neno la shukrani kwa Waziri Jenista Mhagama wa pili kutoka kulia na Naibu Waziri, Stella Ikupa wa pili kutoka kushoto mara baada ya kuzinduliwa kwa Baraza hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo  Andrew Massawe.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Andrew Massawe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Baraza hilo (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF, Juni 2, 2019 Jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Sehemu ya wajumbe wa Baraza hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akizindua Baraza hilo Jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa Watu wenye Ulemavu Josephine Lyengi akielezea jinsi kitengo hicho kinavyohudumia Watu wenye Ulemavu.
Mkalimani wa lugha za alama Baster Mlawa (kulia) akimfafanulia Mwenyekiti Chama cha Viziwi Tanzania Nedrosy Mlawa wa pili kutoka kulia (wenye uziwi) kuhusu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri Jenista Mhagama akitoa mkono wa pongezi kwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija wakati wa hafla ya kuzindua Baraza hilo, Jijini Dodoma.
Waziri wa Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya wajumbe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu.
Waziri Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu mara baada ya kuzindua Baraza hilo Jijini Dodoma. Wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Taifa la ushauri kwa Watu wenye Ulemavu Dkt. Lukas Kija, wa pili kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Stella Ikupa. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Andrew Massawe na kulia ni Katibu Taifa wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA)  Jonas Lubayo. (PICHA  NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages