LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 12, 2019

WASALIMISHA KILO 344 ZA MIFUKO YA PLASITIKI

Wafanyabiashara mbalimbali wilayani Mufindi mkoani Iringa wamesalimisha jumla ya kilo 344 za  mifuko ya Plasitiki  kwa ajili ya kuteketezwa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la  serikali  la  upigaji  marufuku matumizi ya mifuko  hiyo.
Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Alli Hapi jana wakati wa  madhimisho ya  siku ya mazingira  duniani  iliyofanyika katika viwanja  vya mashujaa mjini Mafinga wilani Mufindi  kwa  mkoa wa Iringa, mkuu wa wilaya ya  Mufindi Jamhuri Wiliam  alisema kuwa mifuko hiyo   imesalimishwa katika ofisi za Halmashauri  na  wafanyabiashara  hao kabla  kuanza kwa utekelezaji wa agizo la serikali na uzuiaji wa  matumizi ya mifuko  hiyo.

Mkuu  huyo wa wilaya alisema kuwa wilaya ya Mufindi iliweza kutoa elimu kwa wananchi  wake juu ya zuio la matumizi ya mifuko hiyo na hadi  sasa wananchi  wameanza matumizi ya  mifuko mbadala inayotengenezwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka ndani ya  wilaya  hiyo kwa kutumia  karatasi kutoka  kiwanda cha Mgololo  kilichopo wilayani hapo .

”Wananchi wetu wa Mufindi wameheshimu sana na kupokea maelekezo ya serikali ya kuanza matumizi ya mifuko mbadala lakini mkuu wa suala hili la mazingira ni pana sana na linagusa maisha ya wananchi wetu  tunajua suala la kutunza vyanzo vya maji  tumekuwa  tukilipigia kelele na  suala   hili bado lipo na tumekuwa tukiwapigia kelele wananchi wetu kuhakikisha wanaacha hatua tano kutoka mito pindi wanapofanya shughuli za  kilimo.”

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ali Hapi  mbali ya kupongeza hatua iliyochukuliwa na wafanyabiashara na watumiaji wa mifuko ya plastiki wilayani Mufindi kwa kukabidhi kilo 344 za mifuko  hiyo kwaajili ya kuteketezwa  bado aliziagiza  halmashauri zote za mkoa wa Iringa kuendelea kutoa elimu na kuwachukulia  hatua wale wote ambao wanatumia  mifuko ya plastiki mweupe kwa kufungashia  bidhaa ambazo  hazijawekewa nembo ya ubora  na TBS.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages