Jumla ya watu 89 wameuawa na kujeruhiwa katika maeneo tofauti ya Marekani ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.
Kituo cha takwimu za matukio ya utumiaji mabavu na ukatili wa silaha za moto nchini Marekani kimetangaza Jumapili ya leo kwamba, kwa akali watu 19 wameuawa na wengine 70 wamejeruhiwa katika matukio ya ufyatulianaji risasi yaliyojiri ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita na katika majimbo tofauti ya nchi hiyo inayojinadi kuwa kinara wa amani duniani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, aghlabu ya hujuma hizo za ufyatulianaji risasi zimejiri katika majimbo ya Ohio, Florida, New York, Dakota Kusini, Texas, Michigan, Illinois na California.
Aidha katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, kumeripotiwa matukio 164 ya mashambulizi ya silaha za moto katika majimbo tofauti ya Marekani ambapo katika hujuma hizo watu 48 wameripotiwa kuuawa na wengine 125 kujeruhiwa.
Maelfu ya raia wa Marekani huuawa kila mwaka katika matukio ya mashambulizi ya silaha za moto katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Vitendo vya ukatili wa silaha za moto nchini Marekani vimegeuka kuwa moja ya matatizo makubwa na suguu katika jami ya Marekani ambayo imezoea kuzinyoshea kidole cha lawama nchi nyingine za dunia kuhusiana na ukosefu wa amani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇