Dodoma, Tanzania
Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lisu siyo mbunge tena wa jimbo hilo kufuatia kupoteza sifa za kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.
Spika wa Bunge Job Ndugai ameliambia Bunge leo Ijumaa, Juni 28, 2019 kuwa kufuatia hali hiyo amemwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa kiti cha Ubunge cha jimbo hilo la Singida mashariki kipo wazi.
Spika ameliambia Bunge kauli hiyo wakati akiahirisha Mkutano wa 15 wa Bunge akisema Tundu Lisu ambaye alikuwa Mnadhimu Mkuu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, amepoteza sifa za kuwa mbunge wa jimbo hilo kutokana na utoro kwa kutotoa taarifa ya mahali alipo na kutojaza fomu za mali na madeni.
Amesema, hakumfukuza Lisu bali Katiba ndiyo imemuondoa mbunge huyo ambaye kikao chake cha mwisho kuhudhuria Bungeni kilikuwa cha Septemba 7, 2017 ambapo mchana wa siku hiyo anadaiwa kupigwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika eneo la makazi yake,Area D jijini Dodoma.
Baada ya madai hayo ya kushambuliwa kwa risasi Lisu alipelekwa Hospitali ya Rufani ya Dodoma na baadaye usiku wa siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi Kenya alikokaa hadi Januari 6, 2018 kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji anakodaiwa kuwepo hadi sasa.
Your Ad Spot
Jun 28, 2019
TUNDULISU CHALI UBUNGE SINGIDA MASHARIKI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇