LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2019

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI NA WABUNGE 35 WEMEREJEA NCINI

Spika wa Bunge, Job Ndugai na kundi la wabunge 35 wa Bunge la Tanzania wamerejea nchini leo kutoka Misri walipokwenda kuipa hamasa TaifaStars inayoshiriki AFCON2019.

Spika na wabunge hao pia walikuwa na ratiba ya kuzungukia maeneo mbalimbali ya kihistoria na kiuchumi pamoja na uwekezaji katika michezo yaliyoko nchini Misri.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, William Ngeleja, wabunge hao wamejigharamia wenyewe safari nzima bila kutumia fedha za serikali.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club William Ngeleja amekanusha na Kusikitishwa na taarifa za uzushi zinazo sambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii zinazodai Kwamba Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amewapiga Wabunge wenzake.

Ngeleja ameyasema haya muda katika kikao cha Pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai kwenye ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Wabunge hao kurejea Nchini wakitokea Misri.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages