LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 21, 2019

SMZ KUTUMIA TSH. TRIL 1.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2019/20

Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amewasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, ambayo inatarajiwa kutumia Sh trilioni 1.4194, huku mkazo ukiwekwa katika ukusanyaji wa vyanzo vya ndani vya mapato.

Kati ya fedha hizo, matumizi ya kazi za kawaida ni Sh bilioni 842.4 na Sh bilioni 577.0 ni kwa ajili ya kugharamia Mpango wa Maendeleo. Balozi Ramia alisema Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, imejikita zaidi katika kutegemea makusanyo yanayotokana na vyanzo vya ndani ambayo ni Sh bilioni 976.5.

Alisema ili kufanikisha jukumu hilo kikamilifu, watendaji wa taasisi zinazokusanya mapato ikiwemo Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Bodi ya Mapato (ZRB) watawezeshwa, ikiwemo kupewa mafunzo zaidi ya kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kodi.

Balozi Ramia alisema katika bajeti ya mwaka huu, hakuna ongezeko la kodi mpya, huku lengo ni kuendelea kutoa unafuu kwa wananchi na kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao vizuri. Bajeti hii haina ongezeko la kodi huku lengo ni kutoa unafuu kwa wananchi na wafanyabiashara wafanye shughuli zao vizuri za biashara,"alisema.

Aidha, alisema serikali itafanya marekebisho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) pamoja na kutoza kodi kwa wageni wanaolala katika vyombo vya baharini, ikiwemo boti na meli.

Vipaumbele Mapema Balozi Ramia alivitaja vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambavyo ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Dira ya Maendeleo 2020 ni ujenzi wa jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Zanzibar na Bandari ya Mpigaduri iliyopo Maruhubi Unguja. Alisema hayo ni maeneo muhimu, ambayo serikali inategemea kupata mapato mengi kwa ajili ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi.

Aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba utekelezaji wa mradi wa jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, umesitishwa kwa sasa baada ya kukosa ufadhili kutoka Serikali ya China kupitia Benki ya Exim. Kwamba hatua hiyo imetokana na masharti mapya ya mikopo, yaliyowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

"Huu ni mradi muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya Zanzibar na kushindwa kuutekeleza utaleta athari kubwa kisiasa na kiuchumi," alisema. Nyongeza ya mishahara Aidha, Ramia alitoa habari nzuri kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambao hawakunufaika na nyongeza ya mishahara kwamba watafaidika katika mishahara hiyo.

Alitaja baadhi ya makundi ambayo yatafaidika na nyongeza za mishahara ni kundi la wanasiasa ambao ni wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ambapo jumla ya Sh bilioni 75.7 zimetengwa.

Alisema katika mpango huo, ajira mpya zitatolewa kwa vijana pamoja na kuwapandisha vyeo watumishi wa serikali. Misamaha ya kodi Mapema Balozi Ramia alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020, serikali inakusudia kupitia upya kanuni na vigezo vya misamaha ya kodi vinavyotolewa na ZRB.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages