Kwa mara nyingine Rais Recep Tayyip ErdoÄźan wa Uturuki amesema kuwa, licha ya mashinikizo ya Marekani yanayoitaka inchi yake kuachana na mpango wa kununua ngao ya makombora ya S 400 ya Russia, Ankara haitoachana na azma yake ya kununua ngao hiyo.
Rais ErdoÄźan amesisitiza kwamba Uturuki haina nia yoyote ya kulegeza msimamo kuhusu makubaliano ya ununuzi wa ngao hiyo na kwamba Marekani ni lazima ifahamu vyema msimamo huo. Mkataba wa mauziano ya ngao ya S 400 kati ya Uturuki na Russia yalitiwa saini Disemba 2017. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Uturuki inatakiwa kuipatia serikali ya Moscow kiasi cha Dola bilioni 2.5 kwa ajili ya kupokea ngao nne za makombora ya S 400. Hata hivyo serikali ya Marekani sambamba na kupinga suala hilo, imeionya Uturuki kwamba itaiwekea vikwazo vikali serikali ya Ankara sambamba na kubatilisha mpango wa kuiuzia nchi hiyo ndege zake za kivita za F 35.
Hivi karibuni pia Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki alikadhibisha habari zilizoenezwa kwamba Ankara imesimamisha kwa muda mchakato wa ununuzi wa ngao hiyo ya makombora ya Russia kwa pendekezo la Marekani na kusisitiza kwamba suala hilo halina ukweli. Kwa mujibu wa Aksoy mchakato wa ununuzi wa ngao hiyo ya makombora ya S 400 unaendelea kama ulivyopangwa na wala hakuna suala la kuahirishwa kwake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇