Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na Watumishi wa Idara ya Itifaki katika Wizara yake baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John
Magufuli, kwenye nafasi hiyo tarehe 3
Machi 2019.
Pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi aliwataka Watumishi hao kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu
miongozo na maelekezo mbalimbali pamoja na kuwa wazalendo na kufanya kazi zao
kwa kushirikiana na kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkurugenzi wa Idara
ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Grace Martin na Mkurugenzi wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Katika Wizara ya Mambo ya Nje.
Aidha,
mazungumzo hayo ni mwendelezo wa Vikao vya Prof. Palamagamba John Kabudi na
Watumishi wa Wizara yake, ambapo yamefanyika katika Ofisi ndogo jijini Dar es
Salaam tarehe 04 Juni, 2019
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇