Mtaalamu wa masuala ya kisiasa na mhadhiri wa chuo kikuu nchini Uturuki amesema kuwa lengo la vikwazo na mashinikizo ya Marekani dhidi ya Iran ni kuendeleza siasa za kibeberu za White House za kuzidhoofisha nchi zenye nguvu za Asia Magharibi.
Ali Yaman amezungumzia misimamo ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya Iran ya Kiislamu na kusisitiza kwamba, siasa za Washington kuhusu nchi za Asia Magharibi ni kuziwekea mashinikizo nchi zenye uwezo na zenye ushawishi na ndio maana kwa miaka kadhaa sasa Marekani imekuwa ikitekeleza njama za kujaribu kusambaratisha nafasi muhimu ya Iran katika eneo hilo. Ameongeza kwamba, sababu ya Washington ya kuziunga mkono nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi na kuzua migogoro kati ya nchi za eneo hilo, ni maslahi yake haramu ya kiuchumi na siasa zake za ubinafsi. Amesema, kudhamini usalama wa utawala haramu wa Israel ni kati ya malengo muhimu zaidi ya Marekani akifafanua kwamba, wakati Washington inazitaja shughuli za amani za miradi ya nyuklia ya Iran kuwa ni tishio, utawala katili wa Kizayuni unaendelea kuzalisha silaha za nyuklia na una maghala makubwa ya silaha hizo na za kemikali. Amebainisha kwamba hii leo ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) zimegeuka kuwa ghala kubwa la kuhifadhia silaha za mauaji ya umati za Israel.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa wa nchini Uturuki pia amesema, madai ya viongozi wa Marekani ya kutaka kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayana ukweli na kuongeza kuwa, katika upande mmoja Washington inatekeleza mashhinikizo dhidi ya Iran na katika upande mwingine inaiita Tehran kwenye meza moja ya mazungumzo. Amesema kuwa iwapo Washington itakomesha siasa zake za upande mmoja na ikaingia katika mazungumzo ambayo yatadhamini maslahi ya pande mbili, basi si Iran pekee bali nchi zoye za dunia zitakuwa tayari kufanya mazungumzo na Marekani kwa ajili ya kutatua mizozo mingi iliyopo ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇