Wajumbe wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2020-2021 wachaguliwa.
Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa umechagua wajumbe 5 wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2020 -2021.
Kutoka katika kundi la Ulaya ya mashariki Estonia imechaguliwa kwa mara yakwanza katika historia kuwa mjumbe wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Kutoka katika kundi la Afrika, Tunisia na Nigeria zimechaguliwa kuwa wajumbe. Tunisia hapo kabla imeshawahi kuwa mjumbe wa baraza hilo kwa mara tatu, huku Nigeria imewahi kuwa mjumbe mara moja.
Kutoka katika kundi la Amerika kusini na Karibe nchi ya Saint Vincent na Granadin imechaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mjumbe.
Nchi hizo 5 kuanzia Januari 2020 na kuendelea kwa kipindi cha miaka 2 zitakuwa na majukumu kama wajumbe wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaundwa na wajumbe 15 kati yao 5 ni wajumbe wa kudumu ambao ni Marekani, China, Urusi, Uingereza na Ufaransa.
Kati ya wajumbe 10 waliobaki, wajumbe 5 huchaguliwa kutoka makundi 5 ya kijiografia na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kutumikia kipindi cha miaka 2. Wajumbe 5 waliobaki huchaguliwa kila mwaka.
Nchi za Poland, Peru, Kuwait, Equatorial Guinea na Ivory Coast bado ni wajumb na muda wao utamalizika mwaka huu.
Ili kuchaguliwa kuwa mjumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ni budi kupata theluthi ya kura za wajumbe 193 wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇