Mjumbe wa Umoja wa Afrika yuko nchini Sudan kupatanisha mzozo wa nchi hiyo wakati viongozi wa vuguvugu la maandamano nchini humo wakishutumu jeshi linaloongoza nchi hiyo kwa kufanya ukandamizaji wa kinyama dhidi ya waandamanaji.
Chama cha wanataaluma wa Sudan, ambacho kimekuwa nyuma ya maandamano ambayo yalimuondoa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir kutoka madarakani mwezi Aprili, kimetoa taarifa leo kikisema maafisa wa jeshi wanawakamata na kuwatisha watu ambao wameshiriki katika mgomo wa nchi nzima wiki hii.
Wanaharakati walisitisha mgomo na kampeni ya kutotii sheria wakati Marekani na Ethiopia zikiongeza juhudi za kupatikana suluhisho la amani katika mzozo huo, kufuatia ukandamizaji wiki iliyopita uliofanywa na majeshi ya ulinzi dhidi ya waandamanaji wanodai demokrasia ambapo watu zaidi ya 100 waliuwawa.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇