Nchini Ufaransa, maaandamano ya vizibao vya njano yaendelea na kuingia katika wiki yake ya 32.
Maandamano hayo nchini Ufaransa yalianza mwishoni mwa mwaka 2018 kupinga kupanda kwa bidhaa mahitaji katika serikali ya rais Emanuel Macron ambae alilazimika kuongeza mishahara ya wafanyakazi.
Licha ya mishahara kuongezwa maandamano hayakukoma nchini humo.
Ulinzi uliimarishwa katika maandamano na jeshi la Polisi kwa lengo la kuzuia uhabifu wa mali na wahalifu ambao watakuwa wamejipenyeza katika waandamanaji.
Watu 15 walikamatwa na kuwekwa rumande Orves mjini Paris.
Maandamano hayo nchini Ufaransa yalianza Novemba 17 mwaka 2018 kupinga kupanda kwa bidhaa mahitaji ikiwemo bei za mafuta na kudorora kwa uchumi.
Wizara ya ammbo ya ndani ya Ufaransa imetangaza kuwa watu 11 wamekwishafariki na wengine 4245 wakiwemo askari Polisi 1797 wamejeruhiwa tangu kaunza kwa maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇