Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally wakipeana mkono wa kupongezana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Frelimo, Roquel Silva Samuel (Kulia) mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Mchel na wapigania Uhuru wenzake karibu na Chuo cha Mifugo na Kilimo cha Kaole Bagamoyo, leo. Picha na Elisa Shunda.
Picha zaidi/ Bofya HAPA
NA ELISA SHUNDA, BAGAMOYO.
RAI imetolewa kwa vijana wa kiafrika kushirikiana kwa pamoja katika kuongoza jukumu la mapambano dhidi ya wakoloni mamboleo katika kuyakomboa mataifa yao na Afrika kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Frelimo, Roquel Silva Samuel leo wakati alipotembelea na kuangalia historia ya eneo ambalo lilikuwa hifadhi ya Rais wa Kwanza wa Nchi ya Msumbiji,Samola Machel eneo la Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole ambapo yeye na wasaidizi wake wameweza kuona nyumba aliyoishi mkombozi huyo wa nchi ya Msumbiji na Wenzake,Bwalo la Chakula,Darasa la Mafunzo Mbalimbali na Mbinu za Kivita na Eneo Ambalo kulikuwa na handaki kwa ajili ya uhifadhi wa silaha zao.
''Vijana wa Kiafrika wa zamani akiwemo Rais wa Kwanza wa Msumbiji,Samora Machel waliweza kutumia ujana wao katika ukombozi wa nchi zao hata hata hayati mwalimu Julius Nyerere alianza harakati za ukombozi wa Tanganyika akiwa na umri wa kijana, kwa sasa vijana wa sasa wengi wao ujana wao wanaamini wanautumia vizuri ujana wao baada ya kuona tayari labda washapata kununua usafiri kama pikipiki,gari au nyumba ya kuishi wanaona tayari wameshajikomboa kimaisha;
''mimi nasema hapana vijana wa kiafrika mnapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kuongoza jukumu la mapambano dhidi ya wakoloni mamboleo katika kuyakomboa mataifa yenu katika bara letu la afrika kiuchumi kwa kuwa hawa wanyonyaji na wakoloni wanatunyonya mali zetu katika njia ambazo sisi tunachekelea kumbe ndo wanatuumiza taratibu nchi zao za ulaya zinaneemeka wanaishi kwa raha mustarehe ila utajiri wote wanachukua kwetu afrika nawasihi vijana mbadilike muwe kitu kimoja katika vita hii'' Alisema Katibu Samuel.
Aidha katibu huyo mkuu wa chama cha Frelimo baada ya kutembelea nyumba aliyokuwa akiishi mpigania uhuru wa nchi yao Hayati Samora Machel na Wenzake pamoja na sehemu zingine alisema kuwa chama chake kitashirikiana na chama cha mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha wanarekebisha nyumba hiyo pamoja na kuhakikisha sehemu hizo muhimu katika historia ya nchi yao inabaki kuhifadhiwa ili iwe ukumbusho na utalii kwa wananchi wa Nchi ya Msumbiji,Ulimwenguni na vizazi vijavyo wajue umuhimu na undugu wa kweli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nchi ya Msumbiji.
Akiongea katika ziara hiyo,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk.Bashiru Ally Kakurwa alisema kuwa vita hiyo si vita ya silaha na bunduki bali ni vita ya mshikamano ni lazima wajenge umoja kwanza na akasema wameingia katika mfumo wa vyama vingi lakini bado vyama hivyo havijaisaidia katika kujenga mshikamano wa kitaifa,kimataifa katika Afrika na nchi zote maskini,funzo hatuwezi kushinda vita hiyo bila kuwa na umoja wa kitaifa na umoja wa afrika.
''kazi ambayo hatujafanya sisi kizazi cha sasa ni kuiunganisha afrika ili nchi za bara hilo zifanye biashara,uwekezaji,ziendeshe mashule,tafiti kuhusu kilimo kwa pamoja hatujafika huko,lakini sisi Tanzania tumeanza kuonyesha njia tumefufua shirika letu la ndege na sasa hivi linafanya safari Zimbabwe,Afrika Kusini na baadae nchi zingine,katika ziara ya hivi karibuni ya Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli tumepata masoko ya mahindi katika nchi za Namibia na Zimbabwe;
''Sisi Tanzania kupitia chama chetu cha CCM tumezidi kuweka mahusiano mazuri leo hii Frelimo ya Msumbiji,Swapo ya Namibia,ANC ya Afrika Kusini,MPRA ya Angola na ZANUPF ya Zimbawe vyama sita tunajenga kwa pamoja Chuo cha Uongozi na Siasa cha kisasa pale Kibaha ili vijana na makada wa vyama hivi wajifunze namna vijana wenzao waliopita walivyoshiriki katika mapambano ya ukombozi ndio maana leo pia ugeni huu tulipitia katika eneo hilo linalojengwa chuo hicho'' Alisema Katibu Mkuu CCM Bashiru Ally.
Pia Katibu Bashiru ametoa siku tano kwa uongozi wa Mkoa na Chama Pwani kuleta mpango jinsi ukarabati wa chuo cha mifugo na kilimo kwa sasa ambapo awali Rais wa Zimbabwe,Emerson Mnangagwa alisoma katika chuo hicho kama mpigania uhuru aliacha mchango wa Dola Elfu Sitini ili zisaidie kukarabati sehemu ya majengo ya chuo hicho.
Alisema ni mwaka mmoja sasa bado hajaletewa amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evalist Ndikilo kuhakikisha mpango mkakati wa ukarabati wa jengo hilo na upimaji wa ardhi ya eneo hilo unakamilika ili zoezi la ukarabati uanze mara moja.
Mkutano Huo Umehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Abdallah Haji Haidari,Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Taifa,Erasto Sima,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka,Katibu Jumuiya ya Wazazi Pwani,Gama Juma Gama,Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi Wilay ya Bagamoyo,Abubakar Mlawa,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini,Edwin Shunda,DC Bagamoyo,Zainab Kawawa,Mbunge Chalinze,Ridhiwan Kikwete
Your Ad Spot
Jun 18, 2019
Home
featured
siasa
KATIBU MKUU CHAMA CHA FRELIMO ROQUEL SILVA SAMUEL ASEMA VIJANA WANA JUKUMU LA KUONGOZA MAPAMBANO YA KUIKOMBOA AFRIKA KIUCHUMI
KATIBU MKUU CHAMA CHA FRELIMO ROQUEL SILVA SAMUEL ASEMA VIJANA WANA JUKUMU LA KUONGOZA MAPAMBANO YA KUIKOMBOA AFRIKA KIUCHUMI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Elisa Shunda
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇