Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akizungumza, katika hafla ya kukabidhi kompyuta na printa kwa Makatibu wa Jumuiya hiyo wa mikoa, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Elisa Shunda)
Na Mwandishi wetu Dar
JUMUIYA ya Wazazi Tanzania, ambayo ni jumuiya kongwe ya CCM, imejipanga kuwa na kompyuta na vifaa vyake kwenye ofisi zake mbali mbali nchini ili kudhibiti vyaraka zake muhimu kuvuja.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu was Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima alipokuwa akipokea na kukabidhi 'Printa' na Kompyuta zenye thamani ya jumla ya Sh. Milioni 45, kwa Makatibu kadhaa wa Jumuiya wa takribani mikoa 26.
Alisema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kuboresha utendaji kazi, na kuwa na uhakika wa kutunza usiri wa nyaraka za Jumuiya hiyo na hivyo kuepusha hatari ya kuvuja taarifa za siri, kunakoweza kutokea makatibu wanapolazimika kwenda kuchapa kazi kwa watu binafsi kutokana na ukosefu wa vifaa.
Katibu Mkuu amesema ugawaji uliofanyika leo kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga ni mwendelezo wa ugawaji wa vifaa hivyo kwa kuwa tayri mikoa kadhaa imeshapata vifaa kama hivyo.
Katibu Mkuu Erasto Sima, alisema kuwa sehemu kubwa ya vifaa kama alivyogawa vimekuwa vikitolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Najma Giga, anayetokea Jumuiya ya Wazazi Zanziabar kwa ajili ya kuboresha jumuiya hiyo katika utendaji wa kazi za makatibu wa Jumuiya was mikoa.
Katibu Mkuu amewataka wale wote wanabahatika kupata nafasi kama za Ubunge kwa msaada mkubwa wa Jumuiya kuisaidia Jumuiya Hiyo.
"Leo nimekabidhi vifaa vya kompyuta na printa kwa makatibu wa mikoa mitatu ambapo ni katika muendelezo wa ugawaji wa vifaa hivi kwa watendaji wetu hadi sasa ni mikoa 26 imeshapata vifaa hivi kwa ajili ya utendaji kazi wa ofisi, lakini pia ni njia mojawapo ya kuweka mipango mikakati ya kuhakikisha tunaficha siri za ofisi zetu kwa hatua hii tuliyofikia kuwa na vifaa vyetu ni mojawapo ya mikakati yetu katika uboreshaji wa ofisi zetu mikoani;
"Vifaa hivi vimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu, Najma Giga, anayetokea Jumuiya ya Wazazi kutoka Tanzania Visiwani kama mojawapo ya mchango wake katika jumuiya yetu lakini pia ni njia mojawapo ya sisi kama Jumuiya kufurahia uwepo wa wabunge wa jumuiya yetu lakini pia nipende kumkumbusha na mbunge mwingine anayetokea katika Jumuiya yetu kupitia upande huu wa Tanzania Bara naye atukumbuke katika nyanja mbalimbali kwa jinsi atakavyowiwa ili tuzidi kuboresha utendaji kazi wa urahisi wa jumuiya yetu" alisema Sima.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kompyuta na printa kwa ajili ya ofisi yake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Pwani Juma Gama, aliushukuru uongozi kupitia kwa Mwenyekiti wa Jumuiya Hiyo Dk. Edmund Mndolwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya Hiyo, Erasto Sima kwa kuwapatia vifaa hivyo na kusema kuwa itarahisisha utendaji kazi wa ofisini kwao.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Tanga, Mohamed Mdoe, alisema kuwa kwa kukabidhiwa vifaa hivyo ni njia mojawapo ya kuweka usiri wa kazi za ofisi yao kwa kuwa muda mwingine wanakwenda kuchapa kazi za jumuiya nje na ofisi halafu kutokana na wachapishaji kutokuwa na usiri wa kazi zao na kuvujisha taarifa katika sehemu isiyo husika.
Your Ad Spot
Jun 4, 2019
Home
featured
siasa
JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA YAZIDI KUJIIMARISHA KWA KUGAWA KOMPYUTA NA VIFAA VYAKE MIKOAN ILI KUTHIBITI KUVUJA TAARIFA ZAKE ZA SIRI
JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA YAZIDI KUJIIMARISHA KWA KUGAWA KOMPYUTA NA VIFAA VYAKE MIKOAN ILI KUTHIBITI KUVUJA TAARIFA ZAKE ZA SIRI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇