Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amepiga marufuku kwa wananchi kuingiza mifugo, kupita au kufanya shughuri zozote ndani ya uwanja wa ndege kwani ni kosa kisheria.
Ametoa katazo hilo jijini Hapa wakati wa ziara akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kutembelea uwanja huo na kuona utendaji kazi ndani ya uwanja wa ndege uliopo mtaa wa Makole Jijini hapa amesema ni marufuku kwa mwananchi yeyote kuingia na kufanya shughuri ndani ya uwanja wa ndege kwamba ni kosa kisheria.
Na kuagiza Wizara ya mifugo kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji kuondoa mifugo yote inayozagaa ovyo mjini hasa mbwa, na kwamba ndio inayosababisha kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwamba ni hatari kwa wasafiri wanaotumia uwanja huo na kuagiza kila mwananchi kuhakikisha haruhusu mifugo yake kuzagaa mjini.
“Nimetembele uwanja huu mifugo inazagaa ovyo kama unavyoona hapo tumeona mbwa wako ndani ya uzio hii ni hatari kwa wasafiri na ndege inapopaa na kutua, niagize sasa wizara ya mifugo kuhakikisha mnaondoa mifugo yote inayozagaa mjini na wananchi wahakikishe wanawadhibiti wanyama wao wasitembee ovyo” amesema Katambi.
Aidha amepiga marufuku kwa wananchi kuchoma moto jirani na uwanja huo, akibaini baadhi ya maeneo kuchomwa moto ndani ya uwanja atawawajibisha wale wote ambao wanaishi jirani na eneo ambalo moto huo umetokea, amepiga marufuku kwa waliokuwa wakihujumu miondombinu ya uwanja hasa kwa watengeneza heng’a za nguo kwa kukata senyenge za uzio wa uwanja.
Pia amebaini kuwapo kwa maji ndani ya uzio wa uwanja ambapo watumishi wa uwanja walikuwa wakizani ni chanzo cha maji kumbe ni kuvuja kwa mfumo wa maji ambopo yamevuja kwa mda wa miaka mitatu bila kujulikana.
Na kuagiza mamlaka ya maji Wilaya ya Dodoma Mjini kuhakikisha wanafanya ukarabati wa miondombinu maeneo hayo ili kuondoa kasoro hiyo, amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi kwa upotevu huo wa maji.
Meneja wa ufundi wa DUWASA, Kashirima Mayunga amesema ni mda mrefu sasa wamekuwa wakibaini upotevu wa maji bila kujua ni wapi maji hayo yanapotelea na kuahidi hufanyamarekebisho haraka kuondoa kasoro hizo iili kudhibiti uptevu wa maji.
“Tumekuwa tukipoteza maji na tunaona hasara na upotevu wa uniti za maji bila kujua ni wapi maji hayo yanapotelea tunashukuru kwa kujua mahali maji kwa kiasi kikubwa yanapotelea na tunaahidi kutatua changamoto hii haraka sana” amesema Mayunga.
Nae Subiri Kabuka kutoka uwanja wa ndege amesema kwa mda mrefu wamekuwa wakidhani kuwa ni chanzo cha maji kumbe ni kuvuja kwa mfumo wa maji katika eneo hilo na yamekuwa yakileta usumbufukwa kutaka kuingia katika njia ya ndege na tumekuwa tukiyazuia.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇