Mwenyekiti wa Marefarii Mkoa wa Pwani (Corefa) Dk.Mohamed Kirumo (jezi nyeupe) akiwafundisha waamuzi wa awali wa mpira wa miguu katika mafunzo ya wiki mbili yanayofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Mwambisi Iliyopo Mtaa wa Mwambisi Kata ya Mwambisi wilayani Kibaha leo. Kulia Aliyekaa Mbele ni Katibu wa Waamuzi wa Mpira wa Miguu Mkoa wa PWani,Simon Mbelwa. Picha Zote na Elisa Shunda.
NA:ELISA SHUNDA,KIBAHA
UONGOZI wa Chama Cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) Wameanzisha Mafunzo ya Waamuzi wa Awali katika Mkoa Huo Ambapo Kozi Hiyo Inafanyika katika Eneo la Shule ya Sekondari ya Mwambisi iliyopo Mtaa wa Mwambisi,Kata ya Kongowe.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari Hii leo,Mwenyekiti wa Marefa wa Mkoa wa Pwani,Dk.Mohamed Kirumo alisema kuwa lengo la Corefa kuanzisha mafunzo hayo ni kutengeneza waamuzi wapya ambao watasaidia kuchezesha ligi daraja la tatu lakini pia hata kwenye mashule kukiwa na mashindano itapendeza zaidi marefarii watakaokuwa wakisimamia mashindano hayo wawe na uelewa juu ya sheria za uchezeshaji wa mpira wa miguu.
"Tumeamua kuanzisha mafunzo haya kwa ajili ya kutengeneza waamuzi wapya kwa kuwa hawa waliopo ndio wanaelekea uzeeni watastaafu hivyo ni lazima tuwatengeneze waamuzi wapya lakini pia tulipokea maelekezo kutoka (TFF) kuwa tuandae marefarii ambao tutawatumia hata mashuleni kunapokuwa na mashindano au mabonanza mchezo huo uendeshwe kwa sheria zote za mpira wa miguu" Alisema Mwenyekiti Kirumo.
Aidha Katibu wa Corefa wa Mkoa Huo,Simon Mbelwa alisema kuwa wanajenga waamuzi wapya kwa ajili ya kuchezesha mpira kwa ligi daraja la tatu lakini pia akasema kufanya mafunzo haya ya waamuzi wapya ni njia mojawapo ya kuwasaidia vijana katika kuwatengenezea ajira kwa maana michezo ni ajira na katika ajira hizo pia waamuzi wanaweza kupata ajira katika uchezeshaji wa mpira vizuri endapo watazingatia sheria zote za mpira wa miguu wawapo uwanjani.
"Asikuambie mtu kuna watu mbalimbali vijana na watu wenye rika la kati wanaishi na kuendesha maisha ya familia zao kupitia michezo mbalimbali hivyo basi sisi Corefa Pwani kwa kuanzisha mafunzo haya tunawatengenezea vijana wetu ajira endapo kama watawasikiliza vizuri wakufunzi wao na kufuata sheria za mpira wa miguu wawapo kwenye mashindano ni imani yangu watakua kiuchezeshaji na kuzidi kujitengenezea nafasi ya kusogea mbele kuchezesha mechi za ligi kubwa ndani na nje ya nchi" Alisema Katibu Mbelwa.
Kwa upande wake mmoja kati ya mwanafunzi anayeshiriki kwenye mafunzo hayo ya waamuzi wa awali, Ibrahim Seleman alisema kuwa mafunzo hayo ni mojawapo ya fursa kwa vijana lakini pia ni ajira kama wakijiendeleza vizuri na kuwasikiliza wakufunzi kwa umakini watafanikiwa hadi kuchezesha ligi kubwa.
Naye Mwanafunzi wa Mafunzo hayo ya Uwamuzi wa Mpira wa Miguu,Rahma Pazzi, alisema kuwa sababu kubwa ya kujifunza mafunzo kwanza kujiongezea uelewa wa uchezeshaji wa mpira wa miguu lakini pia kuelelewa sheria za mpira wa miguu itakayompelekea kuwasaidia wachezaji wenzake wa Timu ya Mlandizi Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania ya Wanawake juu ya sheria za mpira kwa kuwa huwa inatokea sintofahamu baina ya wachezaji na maamuzi ya refarii uwanjani na kusababisha vurugu.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kumalizika Juni 11 ambapo kutakuwa na shughuli fupi ya ugawaji wa vyeti vya mafunzo hayo ya awali na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa mpira wa miguu mkoa wa Pwani,Hassan Hassanoo, uongozi wa chama hicho unawakaribisha wadau wote wa mchezo wa mpira wa miguu kujumuika kwa pamoja siku hiyo ya ufungaji wa mafunzo hayo.
Mwishooo.
Email:elisashunda@gmail.com
Cont:0719976633.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇