Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu aondolewe madarakani Aprili 11 mwaka huu.
Bashir alionekana hadharani jana Jumapili, wakati akitolewa gerezani katika mji mkuu Khartoum akipelekwa kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ambaye alimsomea mashtaka ya ufisadi yanayomkabili.
Kiongozi huyo wa zamani mwenye miaka 75 amesomewa shitaka la ufisadi pamoja na shitaka la kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha za kigeni nyumbani kwake kinyume cha sheria.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa maburungutu ya fedha za kigeni yalikutwa kwenye magunia nyumbani mwake baada ya kuondolewa madarakani alikohudumu kwa takribani miaka 30.
Al-Bashir ambaye hajaonekana hadharani tangu alipokamatwa baada ya kuuzuliwa, tayari alikuwa amefunguliwa mashtaka mengine ya kuchochea vurugu na ghasia.
Waendesha Mashtaka wa Sudan pia waliagiza Bashir achunguzwe kwa tuhuma za utakatishaj fedha na ugaidi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇