LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 20, 2019

AWATAKA WASHAURI WAKE KUJIEPUSHA NA MATAMSHI MAKALI

Trump ametoa kauli hiyo katika kikao maalumu na washauri wake ambapo amewataka kujiepusha na matamshi makali dhidi ya Iran au matamshi yoyote yanayohusiana na uamuzi wa Washington kutaka kuishambulia nchi hii. Mtandao wa habari wa Daily Beast umewanukuu viongozi wa ngazi ya juu wa Marekani na vyanzo vingine vya habari kwamba, Trump pia amewataka viongozi wa nchi hiyo kutumia maneno laini zaidi kuihusu Iran. Aidha Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) pia imetoa taarifa ikisema kuwa, haihitaji kuingia katika mzozo wa kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hata hivyo muda punde baada ya matamshi hayo ya viongozi wa Marekani, asubuhi ya leo ndege moja ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani imetunguliwa na jeshi la Iran baada ya kuingia kinyume cha sheria katika anga ya nchi hii.
Baada ya Marekiani kushindwa kuivamia kijeshi Iran, yalazimika kutumia maneno laini
Ofisi Kuu ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kwamba, mapema leo asubuhi jeshi hilo limetungua ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-4 Global Hawk baada ya kuingia katika anga ya Iran katika eneo la Kouh-e-Mobarak katika mkoa wa Hormozgan, kusini mwa nchi hii. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ndege ya Global Hawk ni kati ya ndege za kisasa kabisa za kijasusi za Jeshi la Marekani. Mgongano wa maneno wa viongozi wa Marekani kuihusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unajiri katika hali ambayo kwa mara kadhaa Tehran imesisitiza utayarifu wake wa kukabiliana na hatua zozote za kupenda vita za Washington dhidi yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages