Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimefichua kwamba askari 70 wa nchi hiyo wameuawa katika wiki za hivi karibuni kwenye mpaka wa nchi hiyo na Yemen.
Ripoti zinasema kuwa, licha ya jitihada za Saudia za kutaka kuwaweka wanajeshi wake mbali na mstari wa mbele wa vita vya Yemen na kuwatanguliza mbele mamluki kutoka Sudan, jeshi la Saudi Arabia limeendelea kupata hasara kubwa za mali na nafsi.
Kukiri kwa Saudia kwamba askari wake 70 wameangamizwa katika wiki za hivi karibuni katika vita vya Yemen kumetangazwa huku baadhi ya duru za kujitegemea zikisisitiza kuwa, idadi ya askari wa nchi hiyo waliouawa nchini Yemen ni kubwa sana kuliko ile inayotangazwa kwenye vyombo vya habari vya Saudi Arabia.
Brigedia Jenerali Yahya Sarii ambaye ni msemaji wa Jeshi la Yemen alisema Jumatano iliyopita kwamba, zaidi ya wanajeshi na mamluki 200 wa Saudi Arabia waliangamizwa na wengine kujeruhiwa katika operesheni iliyofanywa na Jeshi la Yemen na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah huko Najran. Ameongeza kuwa makumi ya wengine wameshikwa mateka.
Ripoti zinaseisitiza kuwa baadhi ya mateka hao ni maafisa wa ngazi za juu katika jeshi la Saudi Arabia.
Maelfu ya raia wa Yemen wameuwa, mamilioni wamelazimishwa kuwa wakimbizi na maelfu ya wengine wamejeruhiwa tangu Saudi Arabia, Imarati na waitifaki wao waanzishe mashambulizi dhidi ya taifa la Yemen mwezi Machi mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇