Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa mjini, Silvastory Ngerera amesema kuwa chama chao hakina mpango wa kuandaa mgombea mwenye nguvu ya kupambana na Mbunge wa Iringa mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa bali kimeandaa mgombea ambaye atayetatua kero na shida za wananchi kwa kuziishi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na diwani wa kata ya Kitanzini, Mahadhi Hepautwa amesema lengo la chama hicho ni utekelezaji wa kazi zilizofanywa na madiwani hao tangu walipochaguliwa.
"Nimesikia mtu mmoja akisema kuwa CCM haina mgombea wa kupambana naye, mwambieni Msigwa kuwa CCM haiandai mgombea wa kupambana naye CCM inaandaa mgombea bora wa kupambana na kero na changamoto za wananchi wa jimbo la Iringa Mjini mgombea ambaye atazijua shida za wananchi wa jimbo la Iringa Mjini, ataziishi na zitamchoma kisha atachukua hatua ya kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu,” amesema Ngerera.
Aidha Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa CCM ni chama kikubwa na kina hazina ya wagombea wa kutosha na wanachosubiri ni kusikia wananchi wa jimbo la Iringa wanataka mtu wa aina gani kwa kuwa chama hicho kina watu wenye sifa zote za kugombea na kuchukua jimbo asubuhi na mapema.
"Msigwa anasema anapata siri nyingi za chama chetu, mwambieni kuwa hizo anazopata ni taarifa sio siri, ila leo hii nataka nimpe siri kubwa ambayo hajawahi kuipata, siri hiyo ni kuwa kwa mwaka 2020 CCM Iringa Mjini tumejipanga kwa udi na uvumba Msigwa ni lazima atoke mjini hapa.”

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇